Ndiyo, bado unaweza kutuma ombi. Katika ombi tutakuomba ujichagulie au “thibitisha” ikiwa unahudumu au umeathiriwa kijamii au kiuchumi, na kuathiriwa kupita kiasi na marufuku ya bangi ili kutusaidia kuelewa zaidi kuhusu biashara au shirika linalotuma maombi.
Kwenye tovuti ndani ya sehemu ya “Selection Process” (“Mchakato wa Uchaguzi”) – tumeshiriki orodha ya vigezo tutakavyotumia kutathmini mapendekezo. Athari za marufuku ya bangi ni mojawapo ya mambo ambayo tutazingatia, lakini sio jambo pekee tunalolitathmini kwa maamuzi ya tuzo.