Tafadhali kagua Miongozo ya Kustahiki (Eligibility Guidelines). Mashirika mengi yatastahiki kwa kuwa tunahakikisha mpango huu unafikiwa na kuwafaa watu wengi.

Watumaji ombi lazima:

  • Wawe shirika lililo ndani ya Jiji la
    Portland (yaani, anwani ya Portland)
  • Wawe:
    • Shirika lisilo la faida
    • Biashara ya kuzalisha faida
    • Shirika lenye ufadhili wa kifedha kutoka kwa shirika la 501(c)(3).
    • Shirika ambalo halikupokea Ruzuku ya Reimagine Oregon awali

Iwapo ungependa usaidizi zaidi, tafadhali zingatia kwanza kutembelea ofisi yetu saa 2 PM kila Ijumaa kabla ya kufungwa kwa kipindi cha kutuma ombi la ruzuku; unaweza kupata kiungo cha kujiunga katika saa za kazi kupitia Zoom, chini ya sehemu ya “Tarehe Muhimu” (“Important Dates”) ya tovuti.